WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumatano, 15 Juni 2016

Ureno, Iceland hakuna mbabe Europa 2016

Timu ya Ureno na Iceland zimetoshana nguvu katika Mchezo uliomalizika kwa Timu hizo kugawana alama kufuatia sare ya bao 1-1.
Ureno ilianza kuzitikisa nyavu za Iceland kwa bao la Luis Nani dakika 31 kipindi cha kwanza, na Ice land wakizawazisha bao hilo kupitia kwa Birkir Bjarson dakika 50 kipindi cha pili.

Na katika mchezo wa mapema Austria ikicheza na Hungary , Hungary iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Adam Szalai na Zoltan Stieber na kuongoza kundi F.

Fainali hizi zinatarajiwa kuendelea tena jumatano kwa michezo Mitatu, Urusi itaivaa Slovakia, Romania itachuana na Switzerland na wenyeji Ufaransa itacheza na Albania