WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 16 Juni 2016

CUF watolea ufafanuzi...

Nukuu ya Maalim Seif "Lipumba Asahau Uenyekiti CUF",Yazua Gumzo...CUF Wametoa Ufafanuzi

Baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii June 15 2016 vimeamka na habari yenye kichwa cha habari ambacho kimenukuu Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif akisema ‘Prof. Lipumba asahau uenyekiti CUF’.

June 15 2016 chama cha wananchi CUF kupitia kwa kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi, Salim Bimani amekanusha taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari ambapo taarifa hiyo imesema kwamba Taarifa hii ni uongo na katibu hajaitoaa. Hii ni miongoni mwa propaganda zinazotengenezwa na watu wasio na malengo mema na chama, wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya chama.

Taarifa imeongeza kuwa maoni na msimamo wa Katibu mkuu Maalim Seif ambaye yuko Marekani ni kwamba wanachama wanasubiri maamuzi ya vikao vya chama vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yanayotokea na vitatangaza maamuzi yake kwa wote.

Chama hicho kimetoa Rai kwa wanahabari kuwa makini sana na vyanzo vya taarifa mbalimbali wanavyotumia kupata taarifa hasa mitandao ya kijamii pia wafuate maadili ya uandishi wa habari na kuandika habari kutoka kwenye vyanzo vya uhakika visivyo na shaka.

Aidha CUF imetoa angalizo kwa wanachama wake wote kuwa makini na taarifa wanazopokea na wazithibitishe kwa umakini ili kuwa na uhakika na kuepuka kupotoshwa.