WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Alhamisi, 30 Juni 2016

Agizo la Serikali lawahangaisha Butiama.

Uamuzi huo ulitangazwa juzi katika kikao cha Baraza la madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Magina Magesa alisema unalenga kuhakikisha halmashauri yao inafikia kiwango cha asilimia 80 cha ukusanyaji kodi.

Magesa alisema hatua dhidi ya watumishi wazembe itahusisha kada zote kuanzia kwa mkurugenzi mtendaji, wakuu wa idara na maofisa wote bila kujali nyadhifa zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Damian Katengesya aliwahakikishia madiwani kuwa ofisi yake imejipanga kuongeza makusanyo ya ndani na kuwaagiza watumishi wote kuanzia vijijini  kutekeleza maelekezo hayo ili kuepuka kuchukuliwa hatua za nidhamu.