Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda
haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka
kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya
wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia
barabara maalum za mradi wa DART.
Takwimu hizo zimetolewa na meneja uhusiani wa
mabasi yao -UDART- Bwana Deus Gugaiwa baada ya
kuibuka kwa ajali ya mara kwa mara ambapo amesema
ajali hizo zimesababisha hasara ya zaidi ya shilingi
milioni 94 kwa ajili ya ukarabati hali inayohatarisha
uwezekano wa mradi huo kuwaendelevu.
Akielezea hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaoendelea
kukiuka sheria, meneja uhusiano wa DART Bwana
William Gatambi amesema Dart kwa kushirikiana na
jeshi la polisi, wizara ya mambo ya ndani, Tanroad
pamoja na jiji la Dar es Salaam wako katika hatua za
mwisho za kutayarisha rasimu ya sheria ndogondongo
zitakazo toa adhabu kwa wanaokaidi utaratibu wa
matumizi sahihi ya miundombinu hiyo Dart.