WE ARE UNDER CONSTRUCTION........COMING BACK SOON
Most Popular

Jumapili, 3 Julai 2016

Magufuli: AirTanzania kupaa tena Septemba

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa

''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.

Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.

Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni